Viongozi wa Dunia wakutana Paris katika mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa.mp4

Your browser doesn’t support HTML5

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amefungua mkutano wa viongozi na wataalam mjini Paris Alhamisi juu ya hali ya hewa, wenye lengo la kutayarisha mpango wa kupunguza mzigo wa madeni  kwa mataifa yenye kipato ya chini.

Mkutano huo pia utajadili suala la kutolewa fedha zaidi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kuanza mpango wa mfumo mpya wa fedha duniani.

Mkutano huo wa ngazi ya juu wa siku mbili unawaleta pamoja karibu viongozi 50 katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris ili kujaribu kufikia maridhiano juu ya namna ya kuendelea mbele na baadhi ya mipango ya kimataifa ambayo inasuasua inayosimamiwa na mashirika makuu kama Umoja wa Mataifa, Benki Kuu ya Dunia na G20.