Uchaguzi unafanyika licha ya kuwepo na mlipuko ya ugonjwa wa Covid 19 na kukiwa na wasi wasi ikiwa utafanyika kwa njia ya huru haki na uwazi. Wapiga kura milioni 5.1 wanatazamiwa kumchagua rais mpya pamoja na wabunge wa bunge la taifa na serikali za mitaa mnamo duru hii ya kwanza.
Uchaguzi unaotarajiwa kumweka madarakani kiongozi mpya Burundi baada ya Nkurunziza
Your browser doesn’t support HTML5
Uchaguzi wa Jumatano nchini Burundi utakua wa kwanza wenye ushindani tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 1993, na kufikisha pia kikomo utawala wa miaka 15 wa Rais Pierre Nkurunziza.