Zaid ya watu 58 wauliwa katika shambulizi la Las Vegas

Mwanaume akiwa amemlalia mwanamke kumkinga na risasi wakati watu wengine wakikimbia kutoka katika tukio la shambulizi la risasi huko Las Vegas, Nevada

Watu wakikimbia katika eneo la tukio la shambulizi la Risasi wakati sauti za risasi zikirindima Oct1, 2017 in Las Vegas, Nevada.

Watu wakikimbia kutoka Hoteli ya Mandalay Bay baada ya mshambuliaji kurusha risasi kwa wahudumu wa eneo la tamasha huko Las Vegas, Octoba 1, 2017

Watu wakiwa katika harakati za kutafuta hifadhi kwenye jengo liliokaribu na tamasha la muziki baada ya risasi kusikika zikirindima huko Las Vegas, Nevada.
 

Mwanamke amekaa chini kwenye ukingo wa barabara huko Las Vegas akiangalia watu ambao wamejeruhiwa wakipelekwa hospitali baada ya tukio la shambulizi la risasi katika tamasha la muziki.

Rais Donald Trump akitoa tamko baada ya tukio la shambulizi la risasi huko Las Vegas, Octoba 2, 2017 akiwa ikulu ya Marekani, Washington
 

Polisi wakiimarisha ulinzi katika eneo la tukio la shambulizi la risasi la Las Vegas baada ya tukio.

Polisi wakiwashauri watu kutafuta sehemu ya kujificha karibu na hoteli hiyo ya ufukweni ya Mandalay na Casino wakati shambulizi la risasi likiendelea Jumapili Oct 1, 2017 huko Las Vegas
 

Watu 58 wauwawa na zaidi ya 500 wajeruhiwa katika shambulizi la bunduki Jumapili huko Las Vegas, Marekani.