Takriban wahamiaji 73 hawajulikani walipo baada ya ajali ya boti karibu na pwani ya Libya

Wahamiaji wa kutoka Libya wakiwa kwenye boti hatari kuelekea Ulaya. Picha ya maktaba.

Takriban wahamiaji 73 wameripotiwa kutojulikana  walipo wakidhaniwa kufa  kufuatia ajali ya meli katika pwani ya  Libya ya Jumanne, ukurasa rasmi wa Twitter wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM umeandika.

Watu saba walionusurika walifanikiwa kufika katika ufukwe baada ya kutoka kwenye boti ambayo ilikuwa imebeba takriban watu 80 wanaripotiwa kuondoka Qasr Alkayar mashariki mwa Tripoli kuelekea ulaya, ripoti zimeongeza. Aidha, IOM imeongeza kusema kuwa hadi sasa miili 11 imepatikana na shirika la mwezi mwekundi la Libya pamoja na polisi wa ndani wakati watu saba walionusurika wakiwa wakilazwa hospitalini . Libya imekuwa sehemu kubwa ya njia ya kuondokea wahamiaji wanaotafuta kufika ulaya kupitia njia hatari na jangwa katika bahari ya mediteranian.