Shambulio la guruneti latokea ndani ya kambi ya polisi Garissa

wapiganaji wa Al-Shabab wanaolaumiwa kupanga mashambulizi mengi Kenya

Maafisa wa usalama nchini Kenya wanasema shambulio la guruneti dhidi ya kanisa liliyoko ndani ya kambi ya polisi mjini Garissa limesababisha kifo cha mtu mmoja watu kumi na moja kujeruhiwa baadhi yao wakijeruhiwa vibaya.

Polisi wanasema kasisi wa kanisa la Utawala Interdenominational aliyekuwa afisa wa p[olisi alifariki alipokuwa anatibiwa kutokana na majeraha aliyopata katika hospitali kuu ya Garissa. Wengi kati ya walojeruhiwa walikua maafisa wa polisi na watu wanne walojeruhiwa vibaya wamesafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu. .

Hakuna mtu anaedai kuhusika na shambulio hilo, lakini inafahamika kwamba wanaharakati wamekuwa wakishambulia vito mbali mbali nchini Kenya tangu majeshi ya nchi hiyo kupelekwa Somalia kusaidia kupambana na wanaharakati wa kislamu wa kundi la Al-Shabab.

Mwezi wa Juali, karibu watu 20 waliuliwa katika mashambulio mawili kama hayo dhidi ya makanisa katika mji wa Garissa uliyoko kaskazinimashariki ya Kenya nkaribu na mpaka wa Somalia.