Washiriki wafurahia sherehe za ufunguzi za michezo ya Olimpiki Rio 2016

Mwanamume akiwa amevaa miwani yenye miduara ya nembo ya Olimpiki kabla ya kuingia Maracana, Rio de Janeiro, Brazil, Aug. 5, 2016. (AP Photo/Natacha Pisarenko)

Mashabiki wa Ujerumani wakipiga picha ya pamoja kabla ya sherehe za ufunguzi. (Reuters/Mike Blake)

Mashabiki kutoka Japan na Marekani katika siku ya ufunguzi, Rio de Janeiro, Brazil, Aug. 5, 2016. (AP/Natacha Pisarenko)

Shabiki kutoka Marekani akielekea uwanja wa Maracana kwa sherehe za ufunguzi, Rio de Janeiro, Brazil, Aug. 5, 2016. (AP/Natacha Pisarenko)

Kulikuwa na hali ya furaha na shangwe katika uwanja wa Maracana Ijumaa, August 5 wakati wa ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Rio. Washiriki kutoka nchi 206 walipita mbele ya viongozi 37 wa mataifa mbali mbali katika sherehe zilizoonyesha pia utamaduni wa Brazil katika sanaa.