Rais wa Uganda aonyesha nia kuwania muhula wa sita

Rais wa Uganda Yoweri Museven

Wakati wa hotuba yake amesema kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanywa nchini humo katika muhula wa sita wa urais.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekiri kwamba changamoto kubwa inayokumba serikali yake ni ukosefu wa maji safi kote nchini, ufisadi na ustawishaji wa kilimo.

Akihutubia kongamano la wanachama wa National Resistance Movement, Museveni amesema kwamba ana maono makubwa kwa taifa la Uganda ambayo lazima atekeleze, akitoa ahadi tele kutetea azma yake ya kutaka kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita.

Your browser doesn’t support HTML5

museven azungumza na wapiga kura

Pamoja na mambo mengine Rais Museven pia ameahidi kuwaongezea mishahara watumishi wa umma, kuwajengea nyumba kwenye maeneo ya kazi na kuhakikisha kwamba kila boma linatajirika.

Wakati wa hotuba yake amesema kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanywa nchini humo katika muhula wa sita wa urais.