Raila na viongozi wa ODM waokoa chama kusambaratika

Viongozi wa CORD, raila Odinga (kulia) Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka

Viongozi wa chama kikuu cha upinzani Kenya ODM katika Mungano wa CORD, wameweza kukubaliana Jumatatu baada ya malumbano makali mwishoni mwa wiki wakati wa kuwachagua viongozi wa chama.

Mvutano wao ulitishia kugawika kwa chama kutokana na utaratibu wa uchaguzi na kuwepo na makundi mawili ya viongozi walotafautiana kabisa juu ya mustakbal wa chama. Uchaguzi haukuweza kufanyika na umeahirishwa hadi mwakani.

Your browser doesn’t support HTML5

Mwaura azungumzia mzozo wa ODM


Mbunge anaewakilisha makundi ya watu walio wahache katika bunge la taifa Isaac Mwaurwa, anasema baada ya malumbano hayo ambayo ni shemu ya mchakato wa demokrasia viongozi wamekubali kuunda tume a kuchunguza kwa nini uchaguzi haukuweza kufanyika.

Bw. Mwaurwa anasema tatizo lilitokanana na kutotayarisha vyema uchaguzi huo na mvutano kati ya vijana na wakongw wa chama. Anasema, tume ya watu watano imeteuliwa kufanya uchunguzi na kukiongoza chama hicho hadi kutayarisha uchaguzi utakaofanyika mwakani.