Papa Francis awasihi vijana kujiepusha na rushwa, kufanya kazi kwa bidii

Your browser doesn’t support HTML5

Zaidi ya watu 65,000 walikuwa uwanjani mjini Kinshasa kumkaribisha Papa Francis ambaye aliwaita vijana ambao alisema ni ‘mabingwa wa udugu’ na ‘wenye ndoto ya dunia iliyoungana’ katika siku ya tatu ya ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Papa Francis Alhamisi aliwasihi maelfu ya vijana nchini Jamhuri ya Kidemokrasa ya Congo kufanya kazi kuelekea katika mustakbali mzuri na kujiepusha na rushwa katika nchi hiyo ya kikatoliki, ambayo imegubikwa na ghasia upande wa mashariki.