November 9, 2015

Kundi la wafuasi wa upinzani wakijipiga picha wakati mamia ya watu wakikusanyika nje ya makao makuu ya upinzani licha ya mvua kubwa Yangon Myanmar.

 Mchoraji picha wa Russia Pyotr Pavlensky akisimama baada ya kuwasha moto kwenye mlango wa makao makuu ya huduma za kiusalama FSB ilioridhi KGB.

Mhamiaji akiwa amezirai kutokana na uchovu muda mfupi baada ya kuwasili kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos kwa kutumia mashuwa.

Mtoto wa nyani aina ya orangutan akiwa kwenye boxi la palstiki baada ya kuokolewa kutoka kwa wawindaji haramu kwenye ofisi za polisi zilizoko kwenye eneo la Pekanbaru kwenye jimbo la Riau.

Mfanyakazi wa manispaa apiga kelele wakati akijaribu kurekebisha bomba lililopasuka kwenye barabara iliofurika kwenye mji wa kusini wa Ashkelon, Israel.

Mfanyakazi wa uokozi atafuta waathirika kwenye mkoa wa Bento Rodrigues uliofunikwa na tope baada ya bwawa linalomilikiwa na Vale AS na BHP Billiton Ltd kuvunja kingo zake Mariana, Brazil, Novemba. 8, 2015.

Msichana asimama karibu na mlango akitazama wenzake wakipata chanjo ya polio iliofanywa nyumba kwa nyumba wakati wa kampeni ya kuangamiza ugonjwa huo Sana'a, Yemen.

Wafanyakazi wapita karibu na bango linaloonyesha sehemu ya kati ya mji uliofunikwa na hewa chafu Beijing, China.

Mlinzi wa ligi ya kulinda ndege (LPO) (kushoto) akigongwa kwa upanga iliotupwa na mmiliki wa ploti ambapo mitego ya ndege ilipatikana wakati wa hatua ya kuzuia uindaji haramu wa ndege huko Audon kusini magharibi mwa Ufaransa.

Kijana wa ki-Palestina ajirusha karibu na ufukwe ulioko karibu na mji wa Gaza.

 Mwendesha farasi aanguka kutoka mgongoni mwake kwenye maonyesho ya rodeo wakati wa siku kuu ya Utamaduni huko San Antonio de Areco, Argentina, Nov. 8, 2015.