Utawala wa kijeshi uliokamata madaraka nchini Niger umemtaka mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka ndani ya saa 72, kulingana na ripoti kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya taifa hilo la Afrika magharibi ambayo shirika la habarai la Reuters imeiona leo Jumatano.
Taarifa hiyo ya Oktoba 10, inashutumu Umoja wa Mataifa kwa kutumia mbinu za kijanja zilizochochewa na Ufaransa kuzuia ushiriki kamili wa Niger kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja huo mwezi uliopita pamoja na na mikutano mingine ya kimataifa. Utawala wa kijeshi ulimuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia mwezi Julai, pia umevifukuza vikosi vya Ufaransa pamoja na balozi wake nchini humo.