Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameamuru kusitishwa kwa muda kwa ujenzi wa mradi wa mitambo ya upepo katika milima ya Golan inayodhibitiwa na Israel ambayo ilizua mapigano ya nadra kati ya wakaazi wa Druze na polisi.
Netanyahu alisema Jumamosi jioni kuwa alikubali kusitisha mradi huo wakati wa sikukuu ya Eid al-Adha inayotarajiwa wiki hii, ambayo ina lengo la kuruhusu muda wa mazungumzo ili kumaliza mgogoro huo. Mradi huo unatarajiwa kuanza tena wiki ijayo. Taarifa kutoka ofisi ya Netanyahu ilisema alifanya uamuzi huo kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa maafisa wa usalama.
Druze inapinga mpango huo ambao utaweka zaidi ya mitambo miwili ya urefu wa mita 200 katika ardhi yao. Wamiliki wa ardhi walisema mitambo hiyo itaharibu pato lao la kilimo na kwamba kampuni ya nishati iliyo nyuma ya mradi huo haikushauriana nao kwa nia njema, madai ambayo kampuni hiyo inakanusha.