New Zealand imesema Ijumaa kwamba inapanga kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi kutokana na kuongezeka kwa mivutano kwenye bahari ya Pacific, kwa kiasi kutokana na kuongezeka kwa harakati za kijeshi za China.
Waziri wa ulinzi Andrew Little, amesema kwamba matumizi ya sasa ya ulinzi ni takriban asilimia 1 ya mapato ya kitaifa, akiongeza kwamba yanatarajiwa kuongezwa ingawa hayatafika asilimia 2.
Little amesema kwamba moja wapo ya vipaumbele ni kuondoa meli za kijeshi pamoja na za doria zilizozeeka. Ameongeza kusema kwamba tishio la ndani limeendelea kuongezeka kutokana na masuala kama vile taarifa potofu, mashambulizi ya kimitandao pamoja na ugaidi.
Hata hivyo nakala ya sera iliyotolewa leo na waziri huyo haijaeleza kwa kina hatua zilizopangwa kuchukuliwa, zikitarajiwa kutangazwa baadaye.