Jeshi la anga limesema mmoja wa marubani kati ya watatu waliohusika katika ajali hiyo ya jumamosi asubuhi amefariki dunia
Ndege mbili za Jeshi la Anga la India zimeanguka wakati zikiwa kwenye mafunzo ya kawaida. Jeshi la anga limesema mmoja wa marubani kati ya watatu waliohusika katika ajali hiyo ya jumamosi asubuhi amefariki dunia. Ajali hiyo ilitokea karibu na Morena huko Madhya Pradesh. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa ndege iliyohusika katika ajali hiyo ni ndege ya kivita aina ya Sukhoi-30 na Mirage-2000.