Wasani wa ngoma za utamaduni Kenya walalamika dhidi ya uwonevu

Frisner Augustin akipiga ngoma za asili

Ngoma za asili nchini Kenya hutumika kama kiburudisho kizuri kwa watalii na kuwanufaisha wasanii hao wanaoendeleza utamaduni huo.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Josephat Kioko.


Wasanii wa ngoma za utamaduni nchini Kenya hutumia muziki wao kuwatumbuiza wenyeji pamoja na watalii hasa katika mkoa wa Pwani ambao hutembelewa na wageni pamoja na watalii kutoka mataifa mengine.

Wanasema kutokana na muziki wa kisasa ambao pia unatumiwa na vijana wengi kujitengenezea maisha yao, wasanii hao wa kitamaduni wamekuwa wakidharauliwa na kulipwa fedha ndogo ikilinganishwa na wasanii wanaochipukia.

Baadhi yao wakielezea namna malipo wanayoyapata wanasema “sana sana kama tunalipwa fedha nyingi ni 3,500 sana sana 3,000 gari huwa tunagharimia 1,500."

Wasani hao wanasema kitu kinacowasiadia ni bidhaa wanaowauzia watali. "Sisi huwa tunaenda na vitu kama vile shanga hivi, mikopa, vitu kama hivi ndio huwa vinatu-bost inakuwa kama ile ngoma ni bridge ya kuingia pale hotelini kwenda kufanya nini, kuuza sasa napia wanatuumiza saa kwa kuwa kuna siku unaweza kwenda ukauza na siku nyingine unaweza kukosa kuuza.”