Matumaini makubwa kwa mustakbal wa Somalia: Mahiga

Wasomalia wakipeperusha bendera za Somalia na Uingereza wakati wa maandamano kuunga mkono mazungumzo ya London

Viongozi wa Jumuia ya kimataifa waeleza matumaini ya maendeleo na ustawi kwa Somalia mpya chini ya uwongozi wa Rais Hassan Shiehk Mahamud, kufuatia mkutano wa viongozi kutoka mataifa 50 na mashirika ya kimataifa mjini London, Jumatatu Mei 6 2013.

Akishirika katika kipindi cha "Live Talk" cha balozi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia Augustine Mahiga anasema tofauti iliyopo hivi sasa ni "kwa sababu ya kazi kubwa ilofanywa mnamo miaka mitatu iliyopita kuleta amani na utulivu ndani ya Somalia. Na kuwa na katiba mpya, bunge jipya na hatimae serikali mpya."

Your browser doesn’t support HTML5

Live Talk - Mustakbal wa Somalia


Taarifa ya mwisho ya mkutano wa London imeeleza kwamba huu ni wakati muhimu kwa mageuzi Somalia na kuahidi kuendelea kuisiadia Somalia katika juhudi za kuleta mageuzi ya kisiasa, kujenga vyombo vyake vya usalama na mfumo wa mahakama na sheria pamoja na kuimarisha mfumo wa usimamizi wa fedha na uwazi.

Tarifa imetowa wito kwa jumuia ya kimataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuimarisha uchumi wake na kuwasaidia walopoteza makazi yaio na kulinda haki za binadam.

Waziri mkuu wa uingerza Cameroon amesema maendeleo muhimu yamepatikana katika kuunga mkono mpango wa rais wa Somalia katika kurudisha nchi yake kuwa na umoja tena.