Mshukiwa wa ugaidi apatikana na hatia Mombasa.

Maafisa wa usalama wakishika doria katika mji wa Mombasa, Kenya ambapo mshukiwa wa ugaidi Jermain Grant alihukumiwa.

Mshukiwa wa ugaidi na ambae ni raiya wa Uingereza, Jermain Grant amehukumiwa kifungo cha miaka tisa gerezani kutokana na shutuma za kujaribu kujisajili kama raiya wa Kenya kinyume cha sheria.

Akiwa mbele ya mahakama ilioongozwa na Jaji Martin Muya, Grant amepatikana na hatia tisa miongoni mwazo zikiwa kujaribu kusajiriwa kama raiya wa Kenya kwa kutumia stakabadhi bandia kinyume cha sheria na pia kutoa habari za uongo akitumia majina bandia ya kikenya.

Your browser doesn’t support HTML5

Grant apatikana na hatia ya ugaidi Mombasa

Uamuzi huo wa mahakama kuu umetupilia mbali uamuzi wa awali kutoka kwa hakimu Anastacia Ndung'u aliekuwa amemuondolea mashitaka hayo. Hata hivyo wakili wa mshukiwa Chacha Mwita amelalamikia uamuzi huo akiahidi kukata rufaa kwa kuwa Grant amekuwa kizuizini kwa muda mrefu na kwamba amekua akishirikiana na mahakama vilivyo.