Kanisa katoliki lapata Papa mpya

Vyombo vya habari Vatikan vikisubiru kuchaguliwa kwa baba mtakatifu mpya

Baada ya kura za siku mbili moshi mweupe umetoka kutoka katika kanisa dogo la Sistine huko Vatikan ikiwa ni ishara kuwa kanisa katoliki limpeta kiongozi mpya Baba Mtakatifu. Makadinali wanaokutana Vatikan wamekuwa katika kanisa hilo dogo tangu jana na muda mfupi ulopita moshi mweupe ulionekana ukitoka juu kuashiria wamefikia uamuzi wa kuchagua Baba Mtakatifu mpya. Bado haijafahamika kiongozi huyo ni nani, wakatoliki kote duniani na waumini wa dini nyingine wanasubiri kwa hamu