Mdahalo wa pili wa urais wamalizika Marekani

Rais Barack Obama (R) na mpinzani wake Mitt Romney (L) katika mdahalo wa pili wa urais huko New York, October 16, 2012.

Rais Barack Obama wa Marekani amemueleza mpinzani wake Mitt Romney wa chama cha Republican kwamba mpango wake wa kuendeleza punguzo la kodi kwa matajiri utaongeza nakisi na kero kwa wamarekani.

Rais Obama aliyasema hayo wakati wa mdahalo wa pili wa kuwania nafasi ya urais uliofanyika katika mtindo wa wapiga kura kuuliza maswali na kujibu papo kwa papo-ujulikanao kama Town Hall Meeting, kwenye chuo kikuu cha Hofstra huko New York.

Your browser doesn’t support HTML5

Sikiliza ripoti ya Khadija Riyami, Washington DC


Bwana Romney alimshutumu Rais kwa kutaka kuongeza kodi kwa matajiri. Bwana Romney alisema mpango wake wa kodi utapelekea kuleta ukuaji wa nafasi za ajira na kuwa na bajeti yenye uwiano.

Wagombea hawa wawili walikuwa wakijibu maswali kutoka kwa wapiga kura ambao bado hawajaamua nani wamchague katika uchaguzi mkuu wa nafasi ya urais utakaofanyika Novemba 6.

Sauti ya Amerika-VOA ilifanya mahojiano na mchambuzi wa masuala ya kisiasa bwana Charles Bwenge wa chuo kikuu cha Florida, Marekani na anatoa tathmini yake kuhusu mdahalo huu.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Charles Bwenge wa Florida, Marekani