Mbabe wa zamani wa kivita Liberia anakata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 20

Ramani ya Liberia na nchi jirani inazopakana nazo

Rufaa hiyo ambayo inaanza Jumatano inatarajiwa kudumu hadi mwanzoni mwa Februari pia itaweka historia inaashiria mara ya kwanza kwamba mashtaka makubwa zaidi ya uhalifu dhidi ya binadamu ambapo kesi itaendeshwa nchini Uswizi

Mbabe wa zamani wa kivita wa Liberia atakata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 20 jela kwa uhalifu wa kivita katika mahakama ya Uswizi leo Jumatano, wakati waendesha mashtaka wakipanua mashtaka hayo ili kujumuisha uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Alieu Kosiah alipatikana na hatia Juni mwaka 2021 kwa ukatili mkubwa uliofanywa wakati wa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia ambapo takriban watu 250,000 walikufa kati ya mwaka 1989 na 2003.

Mahakama ya Uhalifu ya Serikali kuu ya Uswisi ilimkuta "na hatia ya kukiuka sheria za vita".

Hukumu hiyo inaonyesha mara ya kwanza kwa raia wa Liberia kuhukumiwa ama katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi au mahali kwingine kwa uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa mzozo huo.

Rufaa hiyo ambayo itaanza Jumatano na inatarajiwa kudumu hadi mwanzoni mwa Februari pia itaweka historia inaashiria mara ya kwanza kwamba mashtaka makubwa zaidi ya uhalifu dhidi ya binadamu ambapo kesi itaendeshwa nchini Uswizi.

Kama ilivyo uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi yau binadamu unahusu ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso na ubakaji lakini badala ya kuwa matukio ya kipekee au ya hapa na pale ni kwa matukio yanayofanywa kwa njia iliyoenea au ya utaratibu maalum.