Mazungumzo ya mzozo wa Burundi kufanyika Tanzania

Rais wa Ugnad Yoweri Museveni , mpatanishi wa mzozo wa Burundi

Serikali ya Uganda ambayo ni mpatanishi mkuu katika maswala ya Burundi imefichua kwamba uamuzi huo umefikiwa kutokana na hali ya kujikokota kuanza mazungumzo ya kumaliza uhasama wa kisiasa nchini humo, huku maafa makubwa yakiendelea kuripotiwa.

Umoja wa Afrika unatazamiwa kutuma nchini Burundi wanajeshi 5,000 kutoka kikosi chake cha dharura, kutuliza ghasia zinazoendelea nchini humo.

Serikali ya Uganda ambayo ni mpatanishi mkuu katika maswala ya Burundi imefichua kwamba uamuzi huo umefikiwa kutokana na hali ya kujikokota kuanza mazungumzo ya kumaliza uhasama wa kisiasa nchini humo, huku maafa makubwa yakiendelea kuripotiwa.

Your browser doesn’t support HTML5

mazungumzo ya Burundi yatafanyika Arusha, Tanzania

Mazungumzo sasa yamepangiwa kuanza tarehe 28 mwezi huu, Mjini Arusha nchini Tanzania.