Mazungumzo ya amani Maziwa Makuu

Marais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila wa DRC (kulia)

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu Mary Robinson ,yuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Alhamis, baada ya kufanya mazungumzo na maafisa wa Rwanda.

Ziara yake inalenga kuhamasisha amani katika eneo hilo. Mjumbe huyo maalumu anatarajiwa kuanza ratiba ya mikutano leo mjini Kinshasa na maafisa waandamizi wa DRC, wabunge na jumuiya za kiraia na baadaye kutembelea mji wa Goma mashariki mwa nchi.

Kabla ya kuwasili kwake huko Kinshasa mwakilishi huyo maalumu alitembelea Brazzaville, ambako alikutana na rais Denis Sassou Nguesso.