Sherehe hizo zilianza karne ya 12 pale wafalme wa Angkor, walipotumia jeshi la kifalme la wanamaji mwanzoni mwa msimu wa uvuvi, ikiashiria mwisho wa baridi ya msimu wa monsoon, na mwanzo wa msimu wa kuvuna. Hata hivyo sherehe hizo zimekumbwa na majanga kwenye karne ya 21.
Sherehe hizo zilisitishwa kwa miaka kadhaa baada ya mkanyagano wa 2010 kwenye daraja dogo, na kuacha watu 347 wakiwa wamekufa. Katika miaka mitatu iliyopita, michezo hiyo haijafanyika kutokana na kiangazi, janga la corona pamoja masuala ya kiusalama wakati wa mikutano ya viongozi wa kieneno kwenye mji mkuu wa Phnom Penh.
Sasa hivi daraja jipya limefungiliwa mahala palipokuwa na lile lililouwa watu miaka 13 iliyopita wakati wa mkanyagano.