Wagombea watano wa upinzani wakiwemo aliyewahi kuwa gavana wa mkoa wa Katanga, Moise Katumbi, wamesema Jumamosi kwamba zoezi hilo halifai kuheshimiwa kwa kuwa lilikumbwa na udanganyifu mkubwa.
Wagombea wengine watano wakiwemo mshindi wa tuzo ya Nobel Denis Mukwege, na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa kampuni ya mafuta Martin Fayulu wameitisha maandamano ya kupinga uchaguzi huo Jumatano wiki ijayo.
Takriban wapiga kura milioni 44 kwenye taifa hilo la Afrika ya Kati lenye utajiri mkubwa wa madini walijiandikisha kupiga kura ya kuchagua rais, wabunge, viongozi wa mabaraza, pamoja na madiwani.
Rais Felix Tshisekedi ambaye anaonekana kuongoza kwenye idadi ya wabunge kulingana na kura zilizopigwa nje ya nchi, anawania muhula wa pili dhidi ya wagombea wengine 18.
Mataifa ya magharibi yameomba kuwepo kwa hali ya utulivu, wakati kukiwa na wasi wasi wa kujirudia kwa ghasia kama zilizotokea muda mfupi baada ya uchaguzi uliopita.