Kiongozi wa zamani wa Amama Mbabazi amejitokeza hadharani

Amama Mbabazi, mgombea wa zamani wa urais nchini Uganda.

Aliyekuwa kiongozi wa kikosi cha usalama cha Amama Mbabazi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Uganda, Christopher Aine, amejitokeza hadharani siku 90 baada ya kutoweka na hata kudhaniwa kwamba alikuwa ameuawa.

Polisi nchini humo walitoa kitita cha shilingi milioni ishirini, pesa za Uganda, kwa mtu yeyote atakeyetoa taarifa zitakazopelekea kujua mahali alipo Aine, akiwa mfu au hai, lakini Aine amejitokeza ghafla hadharani akiandamana na ndugu wa Rais Yoweri Museveni, aitwaye Salim Saleh.

Ifuatayo ni taarifa ya mwandishi wa VOA mjini Kampala, Kennes Bwire.

Your browser doesn’t support HTML5

Taarifa ya kennes Bwire wa VOA, Kampala