Kimbunga Idalia kimetua jimbo la Florida nchini Marekani

Mitaa ikiwa imejaa maji kufuatia kimbunga Idalia kikiwa Florida.

Idalia ilisababisha mvua kubwa huko Florida wakati dhoruba hiyo ikikaribia pwani ya Ghuba katika jimbo hilo na upepo mkali wa kilomita 215 kwa saa. Kituo cha Taifa cha Kimbunga kimesema Idalia kiliongezeka nguvu katika hatua ya 4 kiwango cha pili chenye nguvu zaidi kabla ya kufika eneo la Big Bend.

Jimbo la kusini mashariki mwa Marekani la Florida lilijiandaa Jumatano kwa kimbunga Idalia, ambacho sasa ni kimbunga cha hatua ya nne, huku watabiri wakitarajia maeneo ya pwani kupata dhoruba kali.

Idalia ilisababisha mvua kubwa huko Florida wakati dhoruba hiyo ikikaribia pwani ya Ghuba katika jimbo hilo na upepo mkali wa kilomita 215 kwa saa. Kituo cha Taifa cha Kimbunga kimesema Idalia kiliongezeka nguvu katika hatua ya 4, kiwango cha pili chenye nguvu zaidi saa chache kabla ya kufika kwenye ardhi katika eneo la Big Bend.

Maeneo yaliyoathiriwa moja kwa moja na kuongezeka kwa dhoruba yanaweza kuona athari mita tatu hadi tano juu ya ardhi. Mamlaka ziliamuru kuhamishwa kwa lazima watu katika kaunti nane kufuatia kimbunga hicho, huku watu katika kaunti zingine 14 wakihimizwa kuondoka.

Katika maandalizi ya juhudi za uokoaji na ukarabati, takriban wanajeshi 5,500 wa kikosi cha ulinzi wa taifa wanaandaliwa na zaidi ya wafanyakazi 30,000 wamewekwa tayari kabla ya kuwasili kwa kimbunga hicho.