Kesi ya Ruto kuanza jumanne ICC

  • Mwai Gikonyo

William Ruto akiwa kwenye chumba cha mahakama ya ICC huko The Hague, Uholanzi, May 14, 2013.

Kesi ya naibu rais wa Kenya, William Ruto itaanza Jumanne huko The Hague, Uholanzi kwa shutuma za uhalifu dhidi ya binadamu. Bwana Ruto aliondoka Nairobi Jumatatu kuelekea mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC akisindikizwa na wafuasi kadhaa.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Mwai Gikonyo, Nairobi


Naibu rais anashutumiwa kwa kusaidia kupanga ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 ghasia ambazo ziliendelea hadi mwaka 2008 ambazo ziliuwa zaidi ya watu 1,000 na kuwakosesha makazi zaidi ya watu nusu milioni kutoka kwenye nyumba zao.

Bwana Ruto anashtakiwa pamoja na mtangazaji wa kituo kimoja cha radio mjini Nairobi, Joshua Arap Sang. Wote wanatarajiwa kukana makosa ya mashtaka.