Kenya: Teknolojia ya virtual reality yatumika kuhamasisha utunzaji mazingira

Your browser doesn’t support HTML5

Teknolojia ya Virtual Reality inajulikana imejikita zaidi kwenye michezo ya video. Lakini kampuni moja nchini Kenya inatumia teknolojia hiyo kufundisha watoto wa shule katika maeneo ya kipato cha chini umuhimu wa kutunza mazingira.

Katika darasa moja jijini Nairobi, wanafunzi wamekuwa wakitumia teknolojia ya Virtual reality kujifunza zaidi kuhusu uchafuzi wa plastiki.