Jinsi ya Kuwawezesha Wakimbizi: Kupata Nishati

Kuna zaidi ya watu milioni 68.5 waliolazimishwa kukimbia makazi yao ulimwenguni na zaidi ya milioni 25 kati yao ni wakimbizi, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR).

Vikwazo vinavyowakabili wakimbizi ni vingi ikiwemo changamoto kama vile kupika, taa, kuchaji simu, kuendesha magari na vifaa vingine vya umeme. Uwezo endelevu wa kupata nishati ni suala nyeti kwa sababu nishati inawapa watu uwezo wa kuendeleza mbele maisha yao na kuishi maisha ya bora ya kujitegemea.

Nishati mbadala kama vile umeme wa solar unaweza kuziba pengo lilioko kati ya misaada ya kibinadamu na maendeleo ambayo yanasaidia watu waliolazimika kuhama makazi yao kuweza kujisimamia wao wenyewe.

Sauti ya Amerika (VOA) na Shirika la Moving Energy Initiative (MEI) liliandaa mkutano wa kimataifa ulihudhuriwa na wakazi wa kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na kuhudhuriwa na wataalamu wa nishati mbadala ambao kwa pamoja walijadili suluhisho la kupatikana nishati ya bei nafuu, ya uhakika, endelevu na ya kisasa.