Jeshi la DRC laitaka Rwanda na waasi wa M23 kuondoka maeneo wanayokalia

Your browser doesn’t support HTML5

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) laeleza masikitiko yake kuona waasi wa M23 wanaendelea na mashambulizi dhidi yao. Msemaji wa jeshi anaeleza kuwa waasi wa M23 na jeshi la Rwanda linapaswa kuondoka katika maeneo ya DRC na kurudi kule walikotokea.

Ungana na mwandishi wetu kusikiliza repoti kamili ikieleza hali ya usalama ilivyo katika maeneo mbalimbali ambayo bado yanakaliwa na waasi wa M23. Endelea kusikiliza...