Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre ahukumiwa maisha jela na mahakama maalum nchini Senegal
Your browser doesn’t support HTML5
Mahakama nchini Senegal imemkuta na hatia rais wa zamani wa Chad Hissene Habre na shutuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa vita na mateso na imemhukumu kifungo cha maisha jela. Makundi ya kutetea haki za binadam yamepongeza hatua hiyo wakisema ni onyo kwa viongozi wanaonyanyasa raia wao .