DRC: Walioathiriwa na mlipuko wa Volcano warejea Goma kuanza maisha upya

Your browser doesn’t support HTML5

Waathirika wa volcano katika mji wa Goma ambapo iliwalazimu kukimbia makazi yao baada ya mlima Nyiragongo kulipuka na kusababisha moto ambao uliteketeza nyumba na mali za wakazi waeneo hilo, wameamua kurudi na kuishi juu ya lava za volcano.

Hii ni kutokana na kuwepo shinikizo la kuwataka waondoke kule walipokuwa wamekwenda kujihifadhi, na pia gharama za kukodi nyumba kuwa kubwa.