Dramani Mahama atangaza kuwania tena urais wa Ghana mwaka ujao

Rais wa zamani wa Ghana, John Dramani Mahama

Rais wa zamani wa  Ghana John Mahama Alhamisi amezindua kampeni yake ya kurejea kwenye wadhifa alioushikilia kati ya 2012 na 2017.

Mahama amewania urais wa Ghana mara tatu, mara mbili akishindwa na rais wa sasa Nana Akufo Addo. Kampeni ya Mahama imezinduliwa wakati nchini inakabiliwa na hali ya kudorora kwa uchumi. jambo ambalo linalopewa kipaumbele kwa sasa.

Mamia ya wafuasi wa Mahama walijitokeza kwenye ukumbi katika mkoa wa Volta, ambao ni ngome ya chama cha upinzani cha National Democratic Congress NDC. Akiwa amevalia mavazi meupe, rangi inayoashiria ushindi nchini Ghana, Mahama alisema kwamba hali iya sasa nchini humo inahitaji kiongozi mwenye uzoefu kama yeye.

Ghana inakabiliwa na hali mbaya sana ya kiuchumi na mgogoro wa kifedha miongo kadhaa, wakati kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwaka kimefikia asilimia 53.6 mwezi januari.

Akizungumza na VOA,Peter Mac Manu mwenyekiti wa zamani wa kitaifa wa chama tawala cha New Patriotic NPP, na pia meneja wa kampeni ya rais Akufo Addo, mwaka 2020 amesema kwamba Mahama mwenye umri wa miaka 64 hana chochote kipya cha kuwapa watu wa

Mei 13 viongozi wa chama hicho watakutana ili kuchagua mshika bendera wa NDC kwenye uchaguzi wa Decemba 7, 2024. Mahama atakuwa akishindana na watu wengine watatu akwemo waziri wa zamani wa fedha na gavana wa benki kuu Kwabena Duffuor.