Trump ashutumiwa kuzusha ghasia wakati wa kampeni zake

Waandamanaji wakishangilia baada Donald Trump kuahirisha mkutano katika chuo kikuu cha Illinois, Chicago, March 11, 2016.

Baadhi ya watu wanamlaumu mgombea wa Republican Donald Trump kwa kuchochea ghasia dhidi ya waandamanaji katika kampeni zake jambo lililopelekea kuahirishwa kwa mkutano wake.

Moja wa maafisa katika kampeni za Trump alisema mgombea huyo alikuwa Amewasili Chicago, na baada ya kukutana na maafisa wa polisi akaamua kwa usalama wa maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika katika mkutano wa usiku uahirishwa hadi tarehe nyingine itakayoppangwa.

Trump alikemea ghasia hizo na kusema kuwa waandamanaji wamekiuka haki yake ya kikatiba ya uhuru wa kuzungumza. Trump alitarajiwa kuzungumza na wafuasia wake kabla ya mkutano mwingine huko Illinois Jumanne.

Wakati huo huo mpinzani wake wa karibu Seneta Marco Rubio alitumia muda mfupi kumlaumu Trump kutokana na ghasia zilizozuka Chicago na kusema kuwa , mwenendo wake umechangia katika ghasia .