CUF yatangaza kutomtambua Rais Shein na serikali yake

Kiongozi wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza na wanahabari

Chama cha Wananchi-CUF kimetangaza rasmi kutomtambua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Serikali yake.

Hata hivyo chama hicho kilisema kitashiriki kikamilifu katika zoezi la kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hata kama uchaguzi huo utasimamia na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inayoongozwa na mwenyekiti wake Alhajj Jecha Salim Jecha.

Ifuatayo ni ripoti ya mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA kutoka Zanzibar.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Munir Zakaria wa VOA, Zanzibar

Wakati huo huo mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Zanzibar, Ali Makame alisema kwamba hii sio mara ya kwanza kwa Chama cha Wananchi-CUF kutoa kauli kama hiyo.

Bwana Makame alisema CUF ilishawahi kutoa matamshi ya kutomtambua rais aliyeko madarakani ambaye hakutoa upande wa CUF hapo mwaka 1995 ilitokea hivyo hivyo, mwaka 2000 na 2005 isipokuwa uchaguzi ambao ulifanyika mwaka 2010.

Sauti ya Amerika VOA ilizungumza na Ali Makame, mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Zanzibar.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano ya VOA na mchambuzi Ali Makame wa Zanzibar