Chama cha ANC Afrika Kusini cha kutana kujadili hatma ya Rais Ramaphosa

Your browser doesn’t support HTML5

Viongozi wa chama tawala Afrika Kusini wanakutana kujadili hatma ya rais Cyril rRamaphosa katikati ya kashfa ya rushwa ambayo imepelekea shinikizo ajiuzulu. Ripoti huru ilisema Ramaphosa huenda alivunja sheria kwa tuhuma za kuficha fedha zilizoibiwa katika shamba lake.

Akizungumza siku ya Jumapili, Ramaphosa alisema hatma yake iko mikononi mwa chama tawala cha ANC. Lakini pia alisema kuwa ataipinga ripoti hiyo kupitia mahakama ya katiba ya nchi hiyo.