CHADEMA huwenda kikakata rufaa kesi ya Zitto Kabwe: Baregu

Zitto Kabwe pamoja na wakili wake Albert Msando (kulia) wakiwasili Mahakama Kuu Dar Es Salaam

Chama cha upinzani cha CHADEMA huko Tanzania kinatazamiwa kukata rufaa kutokana na uwamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kukitaka chama kutojadili uwanachama wa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.

Katika uwamuzi wake wa Jumane Januari 7 2014, Mahakama Kuu ilitoa amri kwamba suala la Bw. Kabwe lisijadiliwe hadi kesi ya msingi itasikilizwa na uwamuzi kutolewa.

Your browser doesn’t support HTML5

Profesa Baregu azungumzia kadhia ya Zitto Kabwe


Akizungumza na Sauti ya Amerika, Profesa Mwesiga Baregu anasema viongozi wa chama watakutana na huwenda wakaamua kukata rufaa, ingawa kuna juhudi za kutafuta maridhiano kati ya viongozi wanaovutana ndani ya chama.

Anasema ingawa kadhia hii ndani ya chama inajadilia kitaifa lakini hiyo ni inaonesha uhai wa chama na mchakato wa kidemokrasia unafanya kazi, na wala hadhani kitendo hicho kitadhuru sifa za chama.

Your browser doesn’t support HTML5

Msando wakili wa Zitto azungumza na M. Mgawe


Wakili wa mbunge Kabwe, Albert Msando anasema wameridhika na uwamuzi wa mahakama na hivi sasa wanasubiri kupata hati kwa maandishi kutoka viongozi wa CHADEMA juu ya mashtaka yanayomkabili mteja wake, ili waweze kuyajibu.