Canada yaongoza kwenye uchafu wa hewa kutokana na moto wa msituni

Moshi uliyofunika mji wa Montreal, Canada, kutokana na moto wa msituni.

Moshi kutokana na moto wa msituni unaoendelea nchini Canada Jumapili ulifunika mji wa Montreal na kupelekea hafla nyingi kuahirishwa, wakati mji huo ukiongoza kwenye viwango vya uchafu wa hewa dunaini, kulingana na takwimu za kimataifa.

Kundi la Uswizi la IQAir linalofuatilia ubora wa hewa ulimwenguni limesema kwamba Montreal ilikuwa ikiongoza kwenye hewa chafu kufikia saa 12 asubuhi ya leo kwa saa za huko.

Mashindano ya mbio za Ironman za Montreal yaliahirishwa kutokana na hali ya hewa kua mbaya wakati maafisa wa mji wakiongeza kuwa michezo mingine ya nje kama vile kuogelea pia zimesitishwa.

Canada inakakabiliana na moto kwenye misitu mbali mbali ikisemekana kufikia 465 kote nchini, kulingana na kituo cha kitaifa kinachofuatilia, cha Interagency Forest Fire Center.