Hali tete Uganda baada ya Kizza Besigye kukamatwa

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye. Huku zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Uganda kufanyika, Besigye amekamatwa na polisi hii leo wakati wafuasi wake wakifanya maandamano kwenye barabara za jiji la Kampala.

Huku zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Uganda kufanyika, mgombea wa urais kwa chama cha upinzani Kizza Besigye amekamatwa na polisi hii leo wakati wafuasi wake wakifanya maandamano kwenye barabara za jiji la Kampala. Siku ya Jumatatu BMJ Muriithi alizungumza kwa njia ya simu na mwanahabariwa Sauti ya Amerika, Sunday Shomari, ambaye yuko mjini Kampala na kwanza akamuuliza hali ilivyokuwa baada ya kukamatwa kwa mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akigombea urais wa nchi hiyo kwa zaidi ya mwongo mmoja bila mafanikio. Sikiliza mahojiano hapa….

Your browser doesn’t support HTML5

VOA'S SUNDAY SHOMARI SPEAKS ABOUT BESIGYE'S ARREST