Berlusconi atimuliwa bungeni

Waziri Mkuu wa zamani wa Italy, Silvio Berlusconi

Bunge la Italy limemtimua Silvio Berlusconi aliyehudumu kwa mihula mitatu kama Waziri Mkuu lakini tajiri huyo ameapa kuendelea na siasa.

Seneti ilipiga kura wiki hii kumuondoa katika bunge kwa sababu ya kushitakiwa kwa makosa ya kodi.

Berlusconi alihutubia wafuasi wake Jumatano nje ya nyumba yake Romani Palazzo akiwaambia kuwa ni siku ya kuhuzunikia demokrasia lakini akawasihi kuendelea kuitetea demokrasia.