Live Talk - Tatizo la hongo kwa Wafrika Mashariki

Ramani ya kiwango cha ulaji rushwa katika nchi za Afrika kusini mwa janga la Sahara

Polisi wa Kenya wametangaza kwamba uchunguzi utafanyika kutokana na ripoti za kuwepo na njama inayofanywa na kundi la polisi kukusanya fedha kutoka wamiliki Matatu, Nairobi, ili kutosimamishwa magari yao kutokana na kosa la barabarani.

Inaripotiwa kwamba kuna polisi aliyekuwa akiweka katika akunti ya benki shilinigi 300 000, sawa na dola 3,400 kila siku zilizokusanywa kinyume cha sheria.

Your browser doesn’t support HTML5

Live talk: Athari za hongo Afrika Mashariki


Mkurugenzi mtendaji wa Transperency International, tawi ya Kenya Samuel Kimeu akizungumza katika Live Talk anasema Uganda inaongoza katika watu kutoa hongo huko Afrika Mashariki kutokana na uchunguzi walofanya 2012 ikifuatiwa na Kenya, Burundi na Rwanda.

Paul Kalomo wa Mega Attorney nchini Tanzania anasema hali hii inatokana na ukosefu wa nidhamu na inabidi wananchi wenyewe wachukuwe hatua za kubadili tabia hii.