Afrika: Athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kupanda bei za vyakula na nishati

Your browser doesn’t support HTML5

Athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa zinasababisha uwezo mdogo wa uzalishaji wa wakulima wadogowadogo, huku ongezeko la bei za vyakula na nishati likiendelea kuathiri Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Wataalam wa masuala ya kiuchumi wanasema tatizo hili limekuwa suala linalopaswa kushughulikiwa kwa haraka. Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unavikutanisha vyama vya wakulima kutoka ukanda huo kujadili hali hiyo na vipi wanaweza kuikabili.