Benjamin Netanyahu aruhusiwa hospitali na anaendelea salama; wanasema madaktari

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Taarifa ya hospitali ilisema vipimo vyote vya afya ya waziri mkuu vilikuwa vya kawaida, ikiwa ni pamoja na vipimo vya moyo wake. Kifaa hicho cha ufuatiliaji mapigo ya moyo kimewekwa, hospitali hiyo ilisema, ili kuiruhusu timu ya afya ya Netanyahu “kuendelea kufuatilia  afya yake wa mara kwa mara”

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliruhusiwa kutoka hospitali siku ya Jumapili, baada ya kuwekewa kifaa maalum cha kufuatilia mapigo ya moyo.

Taarifa ya hospitali ilisema vipimo vyote vya afya ya waziri mkuu vilikuwa vya kawaida, ikiwa ni pamoja na vipimo vya moyo wake. Kifaa hicho cha ufuatiliaji mapigo ya moyo kimewekwa, hospitali hiyo ilisema, ili kuiruhusu timu ya afya ya Netanyahu “kuendelea kufuatilia afya yake wa mara kwa mara”.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 73 alilazwa katika kituo cha matibabu cha Sheba mjini Ramat Gan siku ya Jumamosi kwasababu ya upungufu wa maji mwilini. Baadaye Jumamosi, waziri mkuu alitoa taarifa ya video kutoka hospitali, akisema, “Najisikia vizuri sana”. Aliwasihi watu “kutumia muda mcache katika jua” na “kunywa maji kwa wingi”.

Netanyahu alikuwa kwenye mapumziko katika Bahari ya Galilee mahala ambapo joto lilifikia 38 Celsius au 100.4 Fahrenheit.