Katika ujumbe wake wa siku hii iliyobeba maudhui “kuibua uwezi wa Kiswahili katika zama za kidijitali” mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Audrey Azoulay amesema “Kiswahili ni lugha inayozungumza na watu wa zamani na wa sasa. Ikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 200, ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazotumiwa sana, ikijumuisha lahaja zaidi ya kumi na mbili kuu. Kwa karne nyingi, lugha hii ya Kibantu imeibuka kama njia ya kawaida ya mawasiliano katika maeneo mengi ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na Mashariki ya Kati.”
Mahojiano na Hassan Ali
Your browser doesn’t support HTML5
Dunia inapoadhimisha siku ya Kiswahili, Mwandishi Hassan Ali amekua kwa miaka mingi anafunza Kiswahili kupitia matangazo na mafundisho yake yanaambatana na matumizi ya maneno yenye ucheshi ili kuwavutia wasikilizaji wake kutumia Kiswahili sanifu.