Serikali ya Zimbabwe yazindua sarafu ya dhahabu ya kidijitali

Your browser doesn’t support HTML5

Ofisi ya Shirika la Kimataifa la Fedha IMF nchini Zimbabwe ilielezea wasiwasi wake kuhusu sarafu ya digitali na udhibiti wa soko.

Lakini wachambuzi wanasema soko la kubadilisha fedha za kigeni ambalo linadhibitiwa na serikali ndiyo linachochea tatizo. Zimbabwe ilianza kutumia tena sarafu yake mwaka 2019, lakini hivi sasa thamani iko katika zaidi ya 2,000 kwa dola moja ya Marekani kwenye soko la magendo. Serikali ina matumaini ya kuiachia sarafu ya dhahabu ya digitali ambayo itapunguza kushuka haraka thamani kwa dola ya Zimbabwe.