Uhaba wa dola za Marekani nchini Kenya waendelea kuzua hisia mseto kutoka kwa wachumi

Your browser doesn’t support HTML5

Shilingi ya Kenya imeshuka thamani zaidi wiki hii, dhidi ya dola ya Marekani, na sasa inabadilishwa kwa zaidi ya dola 130, huku kukiwa na upungufu mkubwa wa dola za Marekani, unaoelezwa na wataalam kama unaoendelea kuathiri uchumi wa nchi hiyo, na hata uwezo wake wa kulipa mikopo ya kimataifa.