Upinzani nchini Tanzania umeanza rasmi mikutano ya hadhara ambayo ilipigwa marufuku miaka ya nyuma

Your browser doesn’t support HTML5

Maelfu ya wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA walikusanyika katika viwanja vya Furahisha katika jiji la Mwanza lililoko kando ya ziwa Victoria wakiwa wamejipaka rangi ya bluu, nyekundu na nyeupe ya chama hicho kwenye mkutano wao wa kwanza uliohudhuriwa na viongozi wa juu wa CHADEMA