Raia wawili wa Ethiopia wamewasilisha kesi dhidi ya kampuni mama ya Facebook ya META kuhusu matamshi ya chuki kwenye mitandao ya kijamii

Your browser doesn’t support HTML5

Mtafiti wa zamani wa haki za binadamu wa Amnesty International, Fisseha Tekle ni mmoja wa walalamikaji katika kesi iliyowasilishwa Jumatano na mwingine ni mtoto wa profesa wa chuo kikuu, Meareg Amare ambaye aliuawa wiki kadhaa baada ya machapisho kwenye Facebook kuchochea ghasia dhidi yake