Ukraine imesema imechukua udhibiti wa eneo la Lyman

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Ukraine imesema Jumapili kuwa imechukua udhibiti kamili wa Lyman, kitovu cha kimkakati cha mashariki iliokuwa sehemu ya eneo ambalo Rais wa Russia Vladimir Putin wiki iliyopita alidai kinyume cha sheria kwamba eneo hilo ni sehemu ya Russia.

"Lyman imesafishwa," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitangaza katika kanda fupi ya video kwenye mtandao wake wa Telegram.

Russia haikutoa tamko lolote Jumapili kuhusu hatima ya Lyman lakini ilisema Jumamosi kwamba wanajeshi wake wanaondoka katika eneo hilo kwa sababu inahofia vikosi vya Ukraine vinakaribia kuwazingira. Russia ilikuwa imeuteka Lyman mwezi Mei na iliutumia kama kitovu cha kimkakati na usafirishaji kwa operesheni zake kaskazini mwa mkoa wa Donetsk.

Russia kuipoteza Lyman lilikuwa pigo kubwa sana katika uwanja wa mapambano tangu vikosi vya Ukraine mwezi uliopita vilipoingia katika mkoa wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine na kuwarudisha nyuma warussia kuelekea kwenye mpaka wao.