Jeshi la Sudan lapindua serikali ya Mpito

Your browser doesn’t support HTML5

Akilihutubia taifa Jumatatu, Jenerali Abdel Fatah al-Burhan amesema kwamba wanachukua uwamuzi huu “ili kurekebisha njia kukamilisha mapinduzi ambayo Wasudan wanataka.”
Wa-sudan wengi wanasema hawakubaliani na mapinduzi ya kijeshi na kutaka utawala wa mpito kuendelea na kazi zake baada ya Kiongozi wa kijeshi wa baraza la utawala la Sudan Jenerali Abdel-Fatah al-Burhan kutangaza amri ya dharura kote nchini na kulivunjka baraza la utawala wa mpito na serikali. Wanajeshi wamawakamata viongozi wa tano wa serikali pamoja na waziri mkuu Abdallah Hamdok.Wakati huo huo jumuia ya kimataifa ikitoa wito wa kuachiliwa wanasiasa hao.